Burudani

Mrisho Mpoto awapa ushauri wasanii wanaotegemea show

Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto amewataka wasanii wenzie kuacha kutegemea show pekee na kujitengenezea njia nyingine za kujipatia kipato.

Mrisho Mpoto akikamata fursa kwa Waziri Pinda.
Mrisho Mpoto akikamata fursa kwa Waziri Pinda.

Akizungumza na Bongo5 jana, Mpoto amesema kuwa wasanii wanaHitaji kutafuta elimu ya jinsi ya kutumia brand zao.

“Wasanii wanahitaji kutafuta wasomi ili wajue jinsi ya kutumia majina yao kibiashana,” alisema. “Mrisho Mpoto ni brand, ambayo nikiitumia vizuri itaninufaisha sana. Kwa mfano msanii sasa hivi anategemea kupata pesa kwa njia ya show peke yake ili aishi, hafikirii ule muziki anaoufanya ni biashara, yeye anafanya muziki for fun, anategemea show. Kwahiyo show utaenda Mwanza siku 365? Unategemea show ya Mwanza watu wamejazana wamekushangilia, unakaa wiki moja halafu unaenda Mwanza, ina maana ukishaenda Mwanza mara tatu kwa mwezi lazima uhamishe mkoa, kwa sababu mikoa ipo 25 ukishafanya show hizo ina maana hautafanya show tena mpaka mwaka ujao. Kwahiyo wasanii waache kulialia. Mimi nimemwajiri Mkenya ofisini kwangu ili tu anitafutie masoko ya muziki wangu,” aliongeza.

Pia Mpoto amewataka wasanii kuishi maisha yao halisi na kuepuka maisha fake hali ambayo inawasababishia matatizo katika maisha yao.

“Wasanii unakuta jina lake kubwa lakini hana hela, kwenda out kuwasha gari peke yake linaitaji mafuta. Kuna kampani, hawataki kunywa vinywaji vya bei rahisi tena wanataka kuonekana, anataka kuzungusha round, anataka atoe tip, hivi vitu vyote ni expensive vinahitaji pesa. Kwahiyo kuingia na kutoa unaspend a lot of money. Unapataje hizo hela za kuspend bila show? Kwahiyo lazima tuwe na mipango na mikakati ya kutumia rasilimali zetu za muziki pamoja na kukubali kuishi maisha yake halisi,” alisisitiza Mpoto.

“Kwahiyo tukisema kweli huyu mtu ana hela ni kweli ana hela, sio ana hela nje, ndani hana hela. Kuna haja gani ya kumwambia mtu una hela wakati hauna hela? Kwahiyo unaishi maisha ya kujifunga ambayo yanakutaka umaintain. Sawa unaweza ukafanya hivyo kwa sababu ya kiki lakini kwa njia za kupata hela. Kwahiyo kutafuta hela sio lazima uwe na cash, lakini kitendo cha kuwa na mipango na kuwa na hela unaweza ukawaambia watu nina hela, kwa sababu unaona ndio maana kukawa na vision na mission. Ukishakuwa na vision ya kuwa na pesa unaweza ukawambia watu mimi na pesa, kwahiyo wasanii tubadilike.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents