Habari

Mrisho Mpoto afurahishwa hatua ya nchi ya China kupiga marufuku biashara ya meno ya tembo

Msanii wa muziki wa asili nchi, Mrisho Mpoto ambaye pia amekuwa mmoja kati ya wasanii ambao wanatoa elimu kwa jamii juu ya kukomesha suala la mauwaji ya tembo nchini, ameipokea kwa furaha hatua ya nchi ya China kutaka kupiga marufuku biashara ya meno ya Tembo nchini humo.

Mrisho Mpoto akiteta jambo na mmoja kati ya wadau katika matembezi hayo.

Mapema Jumamosi hii katika matembezi ya amani ya kupinga ujangili hapa nchini, Balozi wa China, Lu Youqing alisema nchi ya China ipo kwenye mkakati wa kupiga marufuku biashara ya meno ya tembo na wanatarajia mwishoni mwa mwaka huu biashara hiyo kufa kabisa.

Akiongea na waandishi wa habari kuhusu kauli hiyo, Mrisho Mpoto alisema hatua hiyo ni nzuri na itasaidia nchi mbalimbali duniani kuiga nyayo zao.

“Mimi ni mmoja kati ya wasanii ambao tumekuwa tukihusika sana katika hizi harakati hasa hasa kimataifa zaidi, nimeshasafiri nchi mbalimbali kama mtanzania kupinga mauwaji ya tembo au ujangili ndio maana hata leo nipo kwa baada ya kualikwa na ubalozi wa China kwamba wameona jitihada zangu,” alisema Mpoto. “Kwa hiyo alichokisema balozi kuhusu nchi ya China kupiga marufuku biashara ya meno ya tembo ni kitu kizuri sana kwa sababu huu ni mwanzo kwa China ambao zimekuwa zikisema China ndo vinara wa biashara hiyo kuwa na mtazamo mwingine, lakini pia kupitia maamuzi haya naona sasa biashara hii inaenda ukingoni kama nchi zingine za Ulaya ambazo zimekuwa zikitajwa kufuata msimamo wa China,”

Alisema suala la kupinga ujangili nchini sio suala la mtu mmoja, kila mtanzania ana haki ya kulinda maliasili za nchi kwajili ya kizazi kijacho.

Pia muimbaji huyo ambaye bado anafanya vizuri na wimbo Sizonje, amesema yeye bado ataendeleza mapambano kwa kuanzisha kampeni mbalimbali ambazo zitawafanya watanzania kufichua majangili kwa kuwa ni watu ambao wanatoka katika jamii zetu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents