Mramba, Yona Bado Wapo Rumande

SIKU ya kwanza walipewa masharti magumu ya dhamana; baadaye wakakata rufaa na kushinda, lakini hawakutoka gerezani na Ijumaa kulikuwa na kasoro kwenye hati zao za mali.Jana Hakimu aligoma kushughulikia dhamana kwa kutokuwepo kibali cha Mahakama.

SIKU ya kwanza walipewa masharti magumu ya dhamana; baadaye wakakata rufaa na kushinda, lakini hawakutoka gerezani na Ijumaa kulikuwa na kasoro kwenye hati zao za mali.
Kama ilivyokuwa Ijumaa, mawaziri hao wanaotuhumiwa kwa makosa ya kutumia vibaya ofisi wakati wakiongoza wizara nyeti, walirejeshwa rumande kwa basi ambalo pia lilichanganya watuhumiwa wa makosa mengine ya jinai.

 

Mramba, ambaye alikuwa waziri katika serikali zote nne akiwa ameshika wizara ya fedha katika serikali ya awamu ya tatu, na Yona, ambaye alikuwa waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, wanadaiwa kuipa kampuni ya M/S Alex Stewart mkataba wa kudhibiti madini kinyume cha sheria.

 

Wote wawili wanadaiwa kuwa vitendo walivyofanya viliisababishia taifa hasara ya Sh11.7bilioni na hivyo wanatakiwa kuweka dhamana ya Sh2.9 bilioni kila mmoja, ikiwa ni robo ya kiwango wanachodaiwa kulitia hasara taifa.
“Mimi nafuata taratibu hata jalada lililotoka Mahakama Kuu halina maelekezo yoyote ya maandishi kwamba washitakiwa waletwe leo mahakamani,” alisema Hakimu Hezron Mwankenja jana.
Hakimu Mwankenja alisema washtakiwa hao hawangeweza kushughulikiwa dhamana yao kwa kuwa hati ya kuwapeleka mahakamani ili wahudhurie kesi yao kwa dharura ya dhamana ilikosekana.
Mwankenja alisema kutokana na hali hiyo hawezi kutoa uamuzi wa dhamana kwa sababu washitakiwa hao hawakuwa na hati hiyo (remove order).
Lakini mawaziri hao walishapelekwa mahakamani kuanzia saa 3.00 asubuhi wakiwa kwenye gari namba STK 4373, lakini hawakuingia mahakamani hadi majira ya saa 7:00 mchana waliporudishwa mahabusu.
Majira ya saa 6:00 mchana umati wa watu wakiwemo ndugu wa mawaziri hao na mawakili wao waliingia katika mahakama ya wazi kusubiri kesi hiyo isikilizwe, lakini ghafla wakasikia ndugu zao wamerudishwa rumande.
Wakati wanaondoka mahakamani hapo, Mramba na Yona walichanganywa katika gari moja na washitakiwa wa kesi za uporaji wa fedha kwa kutumia silaha.
Awali Hakimu Mwankenja alitamka kuwa masharti ya dhamana hiyo ni fedha taslimu Sh3.9 bilioni, kusalimisha hati za kusafiria, kutotoka nje ya Dar es salaam na kuwa na wadhamini wa kuaminika, mmoja akiwa ni ndugu wa karibu.
Lakini mawakili wa washtakiwa hao walikata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi uliokuwa ukiwalazimisha kuweka dhamana ya fedha taslimu tu na kutaka waruhusiwe kuwasilisha hati za mali zisizohamishika ambazo zina thamani sawa na dhamana zinazotakiwa na mahakama.
Jaji Njegafibili Mwaikugile wa Mahakama Kuu alikubali hoja zao na kupunguza masharti na kukubali dhamana ya hati ya mali inayolingana na kiasi cha fedha kilichowekwa na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.

Ilibainika baadaye kuwa pamoja na kutamka kiasi cha Sh3.9 bilioni, Hakimu Mwankenja aliandika kiasi cha Sh2.9 kuwa ndicho kilichotakiwa kuwasilishwa.
Kwa maana hiyo, washitakiwa hao wanatakiwa kutoa dhamana ya Sh Sh 2.9 bilioni, kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika na kutotoka nje ya jiji la Dar es Salaam bila kuwa na kibali cha mahakama.
Watuhumiwa hao kw apamoja wameshtakiwa kwa mashtaka matano, huku Mramba akiwa na mashtaka nane zaidi na kufanya akabiliwe na jumla ya makosa 13.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents