Burudani

Mr Nice inasemekana anashoot video 2 Afrika Kusini zenye bajeti ya Tsh milioni 95

Msanii wa Tanzania ambaye alijaribu kwenda kujaribu bahati yake ya kurudisha jina lake kwenye ramani ya muziki kwa kusaini na label za Kenya, Lucas Mkenda maarufu kama Mr Nice inasemekana anashoot video nchini Afrika Kusini.

nice

GHAFLA ya Kenya imeripoti kuwa, Nice ambaye yuko chini ya label ya Candy n Candy Records ya Kenya ambayo ilimsaini baada ya mkataba wake na Grand Pa kuvunjwa, anashoot video za nyimbo zake mbili ‘Akina Mama’ pamoja na ‘Ulisemaje’ nchini Afrika Kusini.

Mtandao huo umeongeza kuwa bajeti ya video hizo ni shilingi milioni 5 za Kenya, ambayo ni sawa na shilingi milioni 95 za Tanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents