Burudani

Mr Nice atoka hospitali baada ya kunusurika kifo katika ajali ya bajaj iliyochukua uhai wa rafiki yake

Weekend iliyopita msanii Nice Mkenda aka Mr Nice alinusurika kifo baada ya bajaj waliyokuwa wakisafiria yeye na rafiki yake kupata ajali jijini Dar es salaam.

nice

Taarifa zinasema kuwa rafiki wa Nice aitwaye Patrick Msondo alifariki pale pale, na Nice kukimbizwa katika hospitali ya Mwananyamala kwaajili ya matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ndugu wa Patrick kupitia XXL ya Clouds Fm leo, amesema mwili wa marehemu Patrick unazikwa leo.

Ameongeza kuwa baada ya Mr Nice kutibiwa aliruhusiwa kutoka hospitali na kwa sasa yuko kwa bibi yake Kibamba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents