Bongo Movie

Mr. Chuzi na Jini Kabula ndani ya action movie!

Wapenzi wa filamu za action za Tanzania (ambazo si nyingi) wanaweza kuwa na uhakika wa hivi karibuni kuona moja iitwayo ‘Dirty Game’.
Inaweza isiwe na action za nguvu kama The Expendables 2 ya Sylivester Stallone, lakini jambo moja la ukweli ni kuwa kutaonekana ‘stunts’ na udare devil mwingi kwenye filamu hiyo.

Baadhi ya scenes za Dirty Game iliyotengenezwa na kampuni ya Tuesday Entertainment Ltd, zimefanyika angani na kwenye bahari ya Hindi.
Akiongea na mtandao wa Filamu Central mkurugenzi wa kampuni hiyo Tuesday Kihangala aka Mr. Chuzi amesema filamu hiyo imemlazimu kuweka bajeti ndefu pengine kuliko filamu nyingi za Tanzania ili kupata kitu bora.

Amesema gharama kubwa zimetokana na uchaguzi wa maeneo ya kuigizia yaani location kwenye filamu hiyo. Ameongeza kuwa filamu hiyo imefanyika ndani ya boti na kwenye ndege na hivyo camera zaidi ya 10 zimetuka ili kuepuka kurudia matukio kwakuwa kufanya filamu angani ni gharama kubwa.
Waigizaji walioshiriki kwenye Dirty Game iliyofanyika Dar es salaam na Zanzibar ni pamoja na Mr. Chuzi, Jini Kabula, Kojack, Mzee Bomba na wengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents