Burudani

Mr Blue: Nimegundua nikitulia hakuna anayeniweza Tanzania

Rapper anayetamba na wimbo ‘Pesa’ amesema alichogundua na kujifunza katika muziki mwaka huu ni kuwa hakuna msanii anayeweza kumfikia hapa nchini kama akiamua kutulia.

Mr Blue (2)

Akizungumza na Bongo5 leo, Blue amesema matokeo aliyoyapata mwaka huu katika muziki wake yamemwamsha usingizini.

“Mwaka huu nimejifunza na kugundua hakuna anayeniweza Tanzania nzima ni kutulia tu na kufanya kazi zaidi,” amesema Blue. “Mwakani nafanya utulivu vizuri kwa sababu naishi maisha mazuri, kwahiyo nitafanya muziki mzuri. Nataka niinvest kwenye kazi yangu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents