Burudani

Mr Blue kumshirikisha Shaa, Master Jay ataitayarisha

Mr Blue anatarajia kumshirikisha Malkia wa Uswazi, Shaa kwenye ngoma mpya. Wimbo utatayarishwa na Master Jay.

10731514_280227272165997_454644360_n

“Unajua nilikuwa sijatulia ila sasa hivi nimetulia kwahiyo mashabiki wangu najua niliwaahidi video, ipo tayari kwahiyo wiki hii inatoka,” ameiambia Bongo5.

“Unajua siku ya Fiesta tulivyokuwa backstage niliongea na Master Jay nikamuomba nifanye naye kazi si unajua Master ye sasa hivi hafanyi kazi, ila nilivyomuomba akaniambia ‘sawa tutafanya’. Wakati naongea naye Shaa naye akaja, nikaongea pia na Shaa akakubali pia. Kwahiyo hiyo ngoma nitafanya na Shaa maana si unajua sijawahi kufanya kazi na Shaa.”

Hivi karibuni Shaa alipost picha kwenye Instagram akiwa backstage na Blue na kuandika:

Kama ka collabo kanahusika hapa… @mrbluebyser1988 #Fiesta2014 #SerengetiFiesta #aboutlastnight

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents