Burudani

Mr Blue kuanzisha ‘Micharazo Foundation’ kusaidia kukuza vipaji vya muziki

Mr Blue aka Kabayser ameanzisha taasisi ya ‘Micharazo Foundation’ itakayoanza kupokea wasanii wapya na pia itakuwa sehemu ya kukuza vipaji vya wasanii wachanga.

Mr Blue
Blue ameiambia Bongo5 kuwa kama yeye alisaidiwa na watu mpaka akafikia alipo sasa, yeye pia ana wajibu wa kufanya hivyo kwa watu wengine.

“Dhumuni kabisa ya hili kundi ni kusaidia,” amesema Kabayser. “Mimi binafsi nimetoka mtaani watu ndo wamenisaidia mpaka nikafika hapa, kwahiyo ninachokiamini hata kama sina msaada wa kumsaidia mtu pesa ila nina uwezo wa kumsaidia mtanzania mwenzangu, kijana mwenzangu na yeye akafahamika kwenye muziki. Itamsadia na yeye kutengeneza maisha yake na hivyo watu watapata ajira, wasanii watakuwa hawafi na njaa,” ameongeza.

“Pia muziki wa rap ni kipaji changu ambacho nakipenda, kwahiyo itakuwa kama sehemu ya kusaidia vipaji vya Tanzania. Ni kama THT. Watu walikuwa wanatuulizia Blue Micharazo iko wapi? Sasa mtaanza kusikia wasanii kutoka Micharazo. Kama kuna watu wana vipaji wanafikiri wanaweza wakajiunga, tunawakaribisha. Maskani yetu ipo Kinondoni pia na Tabata ambako mimi ninaishi. Kwahiyo tunawakaribisha watu wote na hatuangalii pesa, umri wala jinsia. Tunachoangalia pale ni kipaji cha mtu aliyekuja, yaani kama una kipaji kikubwa haki ya Mungu tunaapia kabisa hatutakuacha.”

“Hatuna idadi ya watu tunaohitaji ila tunachokihitaji ni nguvu nyingine kutoka kwa watu wengine ambao wanaweza ili kuja kuilinda Micharazo na kuiwekea mizizi endapo hata sisi kama hatutakuwa vizuri kikazi basi kuna watu watakuwa wanaitetea. Malengo ya Micharazo ni kuanzisha kitu kama foundation kwaajili ya kuokoa muziki wa rap na muziki wa wasanii wa kuimba wenye vipaji vya RnB.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents