Burudani

Mr Blue autaja na kuuelezea wimbo aliurekodi na Sugu

Mr Blue amemshirikisha mbunge wa Mbeya Mjini, Sugu kwenye wimbo wake mpya, Freedom.

blue

Mr Blue ameiambia Bongo5 kuwa wimbo huo unawaamsha watu mbalimbali wameliokosa uhuru wao.

“Huu wimbo umetokea tu, idea imekuja tu,” amesema.

blue-3

“Marco Chali alikuwa na hii beat tangu mwaka 2013 na hiyo idea ya freedom ilikuwepo tu. Chorus ilikuwa imeshapigwa, sasa labda kitu ambacho kimejitokeza sasa hivi si kwa sababu ya uchaguzi au labda kwa sababu nimemshirikisha mwanasiasa Sugu hapana,” amesisitiza.

“Hicho ni kitu ambacho alitengeneza Marco toka mwaka 2013 akawa hajui atampa nani. Lakini bahati nzuri juzi nimekutana naye akaniambia ‘hii kazi inakufaa wewe’ na kwa bahati nzuri tena nipo kwenye mawasiliano na mheshimiwa Sugu kwenye vitu vingine binafsi vya kwenye jamii nikamwingizia hili suala na nikamsikilizisha hii nyimbo akaipenda na akasema yeye inamhusu pia ni kama chakula cha jamii.”

“Nikaona ni jambo zuri kwakuwa nimeanza kumuona wakati nakuwa kisanaa na ni kitu kikubwa kwahiyo ni kitu kilichotokea namna hiyo. Huu wimbo unazungumzia uhuru wa watu, mtu anapapenda nyumbani lakini anaamua kuondoka kwaajili ya vita, kwahiyo huu ni uhuru wa nchi au uhuru wa mtu kwenye nyumba yake. Mtu anaamua kuondoka kutafuta sehemu anayoweza kuishi kwa amani.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents