Burudani

Mr Blue ataja mambo matatu anayojivunia kuwa nayo hadi sasa

April 14 ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa rapper, Harry Sameer aka Mr Blue na wiki hii amezungumza na Bongo5 kuelezea vitu vitatu muhimu alivyovipata hadi sasa.

Blue

1. Kuwa Hai

Mr Blue anaamini kuwa na uhai na afya njema ndio chanzo cha mambo yote. “Namshukuru Mungu kwakuwa bado napumua na nina afya,” amesema.

2. Kuwa na Mtoto

Rapper huyo ambaye jina lake jingine kwenye muziki ni Kabayser amesema mwaka huu imekuwa mara ya kwanza kusherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa baba wa mtoto wa kiume aitwaye Sameer. “Nimesherehekea birthday nikiwa na mtoto na hii ndio mara ya kwanza,” amesema rapper huyo.

3. Kuishi kwenye nyumba yake mwenyewe

Mwaka huu Mr Blue alihamia kwenye nyumba yake mwenyewe na hicho ni kitu anachojivunia zaidi kuwa nacho kwa sasa.
“Nahisi hata kamwili kanaanza kuja vizuri kwakuwa tunamshukuru Mungu utumwa fulani wa kodi umeondoka, maisha yanaendelea mbele.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents