Habari

Mpaka sasa Watanzania 132 wamerudishwa Tanzania kutoka Msumbiji

Idadi ya Watanzania waliofukuzwa nchini Msumbiji imeongezeka hadi kufikia 132, huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka zaidi kutokana na operesheni ya kuwarudisha nyumbani wahamiaji haramu.

Akizungumzia suala hilo leo na wanahabari, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Suzan Kolimba amesema operesheni hiyo haijawalenga Watanzania pekee bali raia wa nchi nyingine walioingia Msumbiji kinyume cha utaratibu.

“Ni kweli watanzania wenzetu wapatao 100 walifukuzwa Msumbiji kupitia Mtwara lakini mpaka sasa wamefika 132 ambao wamefukuzwa kutoka Msumbiji kuja Tanzania, lakini si kwamba tu watanzania lakini pia na nchi nyingine ni kwasababu taarifa ambazo sisi tumefuatilizia kwa kutumia ofisi yetu ya balozi yetu ya Msumbiji ni kwamba zoezi la kuwatoa wageni ambao sio raia wa Msumbiji ambao wameingia Msumbiji si kihalali kwa maana kwamba hawakufuata ule utaratibu. Limefanyika na linaendelea kufanyika kwahiyo ni kama oparesheni ambayo nchi ya Msumbiji imeamua kufanya, kwahiyo katika operesheni hiyo utakuta kwamba watanzania hao 132 mpaka sasa hivi,” amesema Kolimba

Aliongeza “Tunaendelea kufuatilia tuhuma za baadhi ya Watanzania kwamba walifanyiwa ukatili wakati wanarudishwa nyumbani ili tujue hatua za kuchukua. Maofisa wetu wanashirikiana na serikali ya Msumbiji katika kuhakikisha Watanzania hawapati matatizo katika operesheni hiyo.”

Taarifa yake:


Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents