Michezo

Mourinho awajia juu wachezaji wake baada ya ushindi katika FA

By  | 

Kocha wa Manchester United ameanza drama zake za zamani. Ameamua kuwajia juu wachezaji wake kwa kitendo chao cha kushangilia goli la kwanza katika mechi yao ya kombe la FA waliyocheza Jumanne hii dhidi ya Hull City.

Licha ya kupata ushindi wa mabao 2-0 wakiwa katika uwanja wa Old Trafford, Mourinho ameiambia Sky Sports, hakufurahishwa na kiwango cha timu yake katika kipindi cha kwanza na alijiuliza ni kwanini walishangilia goli la kwanza wakati hawakuwa na uhakika wa ushindi.

“We needed to play. In cup ties every goal can be crucial, so why celebrate when you have half an hour to play? I don’t think we should, there is no reason to celebrate the first goal,” amesema Jose.

“Of course, Hull were very well organised like I was expecting and it was not easy for us. But I think we were a bit sloppy. We complicated things, took one too many touches and delayed decisions, giving them time to regroup. In the first half the players had to do better, I had to do better and the fans also could do better,” ameongeza.

Magoli ya United katika mchezo huo yalifungwa na Juan Mata na Marouane Fellaini huku mechi ya pili ikitarajiwa kufanyika katika uwanja wa KCOM Alhamisi ya Januari 26.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments