Michezo

Mourinho anyoosha mikono kwa Bastian Schweinsteiger

Baada ya dhiki ni faraja. Baada ya Bastian Schweinsteiger kujikuta katika wakati mgumu chini ya Jose Mourinho tangu alipotangazwa kuwa kocha wa Manchester United mwanzoni mwa msimu huu, hatimaye kocha huyo ameanza kumnyooshea mikono kiungo huyo.

Akiongea na talkSPORT, Mourinho amesema mchezaji huyo ataendelea kuichezea timu hiyo na sasa atajumuishwa kwenye kikosi kinachoshiriki michuano ya Europa ambapo Man United imeingia katika hatua ya timu 32 bora.

“Ndiyo, atabaki, atakwenda kwenye michuano ya Europa kwa sababu tunafunguliwa nafasi ya Memphis Depay na Morgan Schneiderlin ambao wameondoka wakati wa dirisha dogo. Hatuna wachezaji wengi katika nafasi ya kiungo, hatuna njia nyingi, hivyo ni wazi yeye ni chaguo,” amesema Mourinho.

“Ilikuwa ni nzuri kwake [Schweinsteiger] kurudi na kucheza dakika 90. Ni wazi ilikuwa ngumu kwake kwa sababu hajacheza muda mrefu. Lakini ni muhimu kwake kupata dakika na kujiamini. Tuna mechi nyingi za kucheza – kuna vikombe vingi vya mashindano – tunahitaji kikosi na kila mchezaji kutoa mchango wake,” ameongeza.

Schweinsteiger alifanikiwa kuonyesha kiwango kizuri Jumapili hii katika mechi ya FA walipocheza dhidi ya Wigan Athletics ambapo alicheza dakika zote 90 huku akifanikiwa kufunga goli moja katika ushindi wa mabao 4-0 waliyoupata.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents