Michezo

Mourinho abaki njia panda safari ya Rooney kuhamia China

Kuna kila dalili kwa Wayne Rooney akahamia kucheza soka lake katika ligi ya nchini China maarufu kama Chinese Super League, hiyo inatokana na kauli ya kocha wa Manchester United Jose Mourinho.

Wakati akijibu swali la mmoja ya waandishi wa habari kuhusu kuondoka au kubaki kwa mchezaji huyo ndani ya timu hiyo, Mourinho alisema, “Itabidi umuulize mwenyewe. Siwezi kukuhakikishia kama nitakuwa hapa wiki ijayo sasa vipi nikuhakikishie hata kuwa hapa msimu ujao?”

“So you have to ask him if he wants to stay at the club for the rest of his career or if he sees himself moving on. I’m happy to have him. I have been very open with you. I don’t want him to leave,” ameongeza Mourinho.

Dirisha la usajili la ligi ya China linatarajiwa kufunguliwa Jumanne ya February 28 wiki ijayo ambapo imedaiwa kuwa timu moja ya ligi hiyo imemuahidi kumlipa Rooney mshahara wa paundi milioni 35 kwa mwaka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents