Burudani

Morali ya biashara na ujasiri wa kufanya miradi mipya kwa wasanii wetu ifufuliwe!

50 Cent amesaini mkataba mpya wa miaka miwili na kituo cha runinga cha Starz kubuni miradi mipya na wakati huo huo akiendelea kuwa producer wa tamthilia ya Power.

dcl110292LARGE

Jay Z anasherehekea mtandao wake wa kusikiliza muziki, Tidal kufikisha watumiaji milioni moja na mwezi huu atapiga show kali jijini New York ambayo mapato yake yataenda kwenye charity. Nicki Minaj anatarajiwa kutayarisha na kuongoza series kuhusu maisha yake kupitia ABC Family.

Hiyo ni mifano michache tu ya wasanii wa Marekani wanaotumia majina yao na umaarufu wao kufanya kitu cha ziada ambacho kitawaingizia fedha pia.

Wasanii wetu wanafanya nini ili kujiongezea kipato? Nafahamu kuwa wapo kadhaa wanaofanya miradi midogo midogo kama vile biashara za maduka ya nguo na bidhaa zingine, kumiliki bajaj na mingine. Lakini hizo ni biashara ambazo mtu yoyote anaweza kufanya kwahiyo sio vitu vya kushangaza.

Ni biashara au miradi gani ambayo kupitia brands zao na kujulikana kwao nchi nzina wanazifanya? Mfano mzuri ni Jokate Mwegelo alivyoanzisha brand yake ya Kidoti ambayo inahusiana moja kwa moja na yeye mwenyewe.

Lady Jaydee na Wema Sepetu walioanzisha reality show zilizopata wadhamini wanaowalipa fedha nzuri. AY alivyoshirikiana na akina Salama kuanzisha kipindi cha Mkasi ambacho licha ya kuwapa mkwanja mrefu kupitia sponsors, kimeshinda mara mbili mfululizo tuzo ya kipindi cha runinga kinachopendwa kwenye Tuzo za Watu.

Weusi pia kupitia brand yao nguo imekuwa ikiwaingizia chenji za hapa na pale za kutunisha mfuko. Kuna wasanii pia kama Vanessa Mdee, Diamond, na wengine wachache ambao brands zao zinawaingizia fedha kupitia endorsements za makampuni.

Wengine wanafanya nini kutumia umaarufu wao kufanya miradi mingine iwape mkwanja? Nimpongeze Nahreel kwa wazo lake la kuanzisha shule ya muziki ya The Industry. Inaweza kuanza taratibu lakini mbele ya safari ina uwezekano mkubwa wa kuwa kitu kikubwa pia.

Ninatamani sana kuona wasanii wenye majina hapa nchini wakianza kufikiria nje ya box na kufanya vitu tofauti pia. Kwa Marekani ambako soko la muziki ni thabiti zaidi, mastaa wamekuwa wakiwekeza sana kwenye biashara hususan za mavazi, filamu, vipindi vya TV, vilevi, vilabu vya starehe, teknolojia na electronics na wengine hadi kwenye michezo.

Hatuwezi kufanya kwa kiwango kama chao, lakini kuna baadhi ya vitu vinawezekana japo kinachohitajika ni ubunifu, kuumiza kichwa na kufanya bila kuhofia kushindwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents