Burudani

Mona Gangster asema Young Killer amebadilika, ‘ameshikwa masikio na watu’

Producer wa Classic Sounds, Mona Gangster amesema msanii wake Young Killer amebadilika kama wimbo wake mpya ‘Umebadilika’ ulivyo.

20131223_144845
Young Killer na meneja wake, Mona G

Akiongea na SamMisago.com, Mona amesema kuna watu waliompa maneno ya sumu rapper huyo wa ‘Dear Gambe’ na sasa hamheshimu tena.

“Young Killer amebadilika,amekuwa maarufu na, bado nina mkataba na Young Killer mpaka December 2014 ila anaukiuka mkataba huu kwa kwenda kufanya kazi studio zingine na sasa hata Classic Sounds hafiki,” amesema producer huyo.

“Classic Sounds haimbani msanii ila akitaka kufanya kazi nje ya studio hii ni lazima tubaki kama Executive Producer wa kazi hio ilituhakikishe kiwango cha kazi ni bora, Young Killer amefanya kazi nje ya studio bila taarifa wakati mkataba wa Classic Sounds hauruhusu hicho kitu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents