Habari

Mohammed Dewji achukua mkopo wa shilingi bilioni 434 kukuza himaya yake!!

Mfanyabiashara na mwanasiasa maarufu nchini, Mohammed ‘Mo’ Dewji amechukua mkopo wa dola milioni 260 (zaidi ya shilingi bilioni 434) kutoka kwa benki mbalimbali kuimarisha kampuni yake ya METL.

Mo-Dewji

Wiki mbili zilizopita, kampuni yake ya Star Oils Limited ambayo ni sehemu ya METL Group ilipokea mkopo wa dola milioni 60 kutoka kwa benki ya NBC, Barclays Bank ya Mauritius na ABSA. Star Oils ni kampuni ya mafuta.

Pia wiki mbili zilizopita Dewji alipata mkopo kutoka kwa benki ya Afrika Kusini, FirstRand wa dola milioni 200.
Dewji ameiambia Forbes kuwa anataka kutengeneza ajira 100,000 na kutengeza biashara ya yenye mapato ya dola bilioni 5.

Mohammed Dewji, ni miongoni mwa watu matajiri zaidi barani Afrika ambapo hadi sasa utajiri wake unafikia dola milioni 500. Kampuni yake ya METL ni miongoni mwa makampuni ya kifamilia makubwa zaidi na huingiza zaidi ya dola bilioni 1 kila mwaka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents