Habari

Mohamed Farmaajo achaguliwa kuwa Rais mpya wa Urais Somalia

Waziri mkuu wa zamani wa Somalia, Mohamed Abdullahi Mohamed Farmaajo amechaguliwa kuwa Rais mpya wa tisa atakayeiongoza nchi hiyo.

Farmajo alipata kura 184 ambazo alipigiwa na wabunge wa nchi hiyo huku wapinzani wake Hassan Sheikh akipata kura 97 na Rais wa zamani Sharif Sheikh Ahmed akipata kura 46. Hata hivyo Hassan Sheikh alikubali kushindwa katika uchaguzi huo na Farmajo aliapishwa muda mfupi baadae.

Ushindi huo wa Farmajo umeonekana kumfurahisha Fadumo Dayib ambaye alikuwea mwanamke wa kwanza wa Somalia kutangaza kuwa angewania Urais huo japo baadaye alijitoa.

Nchi ya Somalia inakabiliwa na vita vya kikabila pamoja na vile vya ukoo na haijafanikiwa kufanya uchaguzi wa kidemokrasia unaoshirikisha wananchi kwa kupiga kura tangu 1969 huku wabunge ndio wakipata nafasi ya kuchagua rais wa nchi hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents