Burudani

Mo Music amsifia Barakah Da Prince, azungumzia siri ya kufanikiwa kwa ‘Basi Nenda’ (Audio)

Muimbaji wa ‘Basi Nenda’, Mo Music amemsifia muimbaji mwenzie kutoka Mwanza, Baraka Da Prince, ambaye kwa wengi ameonekana kuwa mpinzani wake.

baraka

Akiongea na kituo cha redio cha Mbeya kwenye kipindi cha Bomba Base Show, Mo Music alisema kila mmoja anafanya vizuri kwa upande wake. “Kila mtu ana mwonekano wake na mtizamo wake na reality inaonekana, anyway anafanya vizuri Baraka, nafanya vizuri kwa upande wangu,” alisema.

Kwa upande mwingine Mo Music amesema mipango mizuri aliyokuwa nayo toka awali ndio imeifanya ngoma yake kuwa kubwa na kutochokwa mapema na mashabiki wa muziki Bongo. “Unajua kila kitu kinakuwa na mipango, ukifanya kila kitu kwa strategies lazima utafika katika malengo yako. Kwahiyo ‘Basi Nenda’ ilikuwa na mipango kabla haijatoka kwahiyo mipango mizuri imesababisha basi nenda kuwa kubwa kiasi hiki,” alisema.

Msikilize hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents