Burudani

Mo Music adai ukubwa wa ‘Basi Nenda’ unampa wakati mgumu ‘wanasubiri narudije’

Hitmaker wa ‘Basi Nenda’, Mo Music amedai kuwa ukubwa na wimbo huo unampa wakati mgumu kwakuwa watu wengi wanasubiri ujio wake wa pili utakavyokuwa.

Moe Music nae atakuwepo

Mo Music ambaye ni mmoja wapo kati ya wasanii watakaofanya show ya Serengeti Fiesta 2014 mkoani Tanga Jumamosi hii, amedai kuwa ana nyimbo zaidi ya tatu lakini bado anaangalia upepo wa muziki unaendaje.

“Unajua watu wameshakuwa na presha kubwa sana kujua mimi nakujaje,” ameiambia Bongo5. “Hicho ndo wananifanya sitaki nikurupuke kutoa track kwa muda ambao wao wanataka. Nataka nifanye kama surprise. Kitu kikubwa mashabiki wakati mwingine huwa wanachanganya sana usipotumia akili. Kila mtu anataka nitoe nyimbo kwa wakati anaohitaji yeye lakini wanashindwa kukumbuka kwamba kila kitu kinaenda kwa strategy.”

“Nyimbo ziko tayari na si moja kuna nyimbo kama 3,4,5, ambapo mpaka sasa hivi tunaangalia tu ipi iende, zipi zibaki. Lakini kila nyimbo ipo katika mahadhi yake tofauti, hatutaki tulinganishe nyimbo ifanane na ‘Basi Nenda’ kwasababu mtoto wa kwanza huwa hafanani na mtoto wa pili na wa tatu, labda wawe mapacha. Ila cha msingi ni ‘Basi Nenda’ itabaki kuwa ‘Basi Nenda’ na nyimbo inayokuja itabaki kuwa inayokuja na yenyewe itachukua mrengo wake katika nafasi inayokuja. Itaweza kuipita hata’Basi Nenda’ katika mahadhi yake. Kwahiyo mimi ninachoangalia sio kuifata ‘Basi Nenda’ naangalia ni kufuata maandishi mazuri, melody nzuri na beat nzuri, hicho ndio wanachokitaka watanzania.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents