Michezo

Mo Dewji kuificha Simba mikononi mwa Juventus ya Italia

Mohammed Dewji amepanga kuiunganisha Simba kwa Juventus ya Italia.

Tajiri huyo namba moja kwa sasa hapa nchini alitua Italia katika klabu hiyo mapema wiki hii na kufanya nao mazungumzo juu ya kuinua soka la Tanzania. Akiongea na mtandao wa Salehjembe, Dewji amesema, “Wiki hii nilifanya kikao na Juventus FC. Wanayo nia ya kuendeleza soka kwa vijana wa Tanzania. Ninatazamia kuitambulisha timu hiyo ya Italia kwa uongozi wa Simba SC ili waanze majadiliano ya jambo hilo.”

Juventus imekuwa ikishirikiana na baadhi ya nchi za Afrika katika kuendeleza mchezo huo ikiwemo Libya (wakati ikiwa tulivu), Tunisia, Morocco na Misri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents