Promotion

Mkuu wa wilaya Temeke ashauri Vodacom kusambaza zaidi huduma kwa wateja wake

Mkuu wa wilaya ya Temeke, Sophia Mjema ametoa ushauri kwa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom kufungua zaidi vituo vya kutoa huduma kwa wateja wilayani humo ili kuwawezesha wateja wake kupata huduma kwa karibu badala ya kuzifuata mbali na kupoteza muda mwingi ambao wangeutumia kufanya shughuli za uzalishaji.

001.MBAGALA
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Shophia Mjema wa kwanza (kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Mbagala zakiemu jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkuu wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo Richard na Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.Hafla hiyo imefanyika leo

Alitoa ushauri huo wakati akifungua duka la Vodacom la Mbagala ambapo pia alitoa pongezi kwa hatua hiyo. Katika kuhakikisha wakazi wa vitongoji vya Mbagala na maeneo jirani ya Mtoni,Temeke na Tandika wanapata huduma kwa karibu,Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom leo imefungua duka jipya katika eneo la Mbagala Zakiemu.

Mbagala ni moja ya kitongoji maarufu katika cha jiji la Dar es Salaam ambacho kinakuwa kwa kasi kwa maendeleo na kuwa kivutio cha wawekezaji wengi kutokana na kuwa na idadi kubwa ya
watu na shughuli mbalimbali za kibiashara ikiwemo kituo kikubwa cha mabasi yanayoelekea mikoa ya Kusini ya Lindi na Mtwara.

Duka hilo jipya lenye mazingira rafiki kwa wateja litakuwa linatoa huduma mbalimbali kwa wateja wa Vodacom ikiwemo huduma kwa mawakala wa Mpesa na uuzaji wa bidhaa za Vodacom na litawawezesha wateja wa Mbagala na vitongoji vyake wakiwemo wasafiri wanaoelekea mikoa ya Kusini na wateja kutoka maeneo ya Temeke,Kurasini,Mtoni na Tandika.

Mtandao wa Vodacom unaongoza kwa kupatikana vizuri na umeenea sehemu zote katika wilaya ya
Temeke.Hassan Saleh Ofisa Mkuu wa Mauzo na Usambazaji Vodacom Tanzania,alisema ufunguzi wa duka hili la kisasa ni mwendelezo wa malengo ya Vodacom kuendeleza kuboresha maisha murua kwa kila mtanzania kwa kupata huduma za kampuni hiyo zenye ubora na kuwafikia wateja kwa urahisi zaidi popote pale walipo ikiwemo huduma mpya ya kilimo klabu inayolenga kuwawezesha wakulima nchini.

“Uzoefu na utafiti umetuonyesha kuwa wananchi wanataka ubora,kama mtandao unaoongoza nchini
tumejizatiti kuhakikisha tunafanya ubunifu wa hali ya juu wa kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo kutoa huduma bora na ndio maana tunazidi kufungua maduka kama haya kwa ajili ya kuwasogezea karibu wananchi huduma bora,na ninawahakikishia kuwa popote wateja wetu walipo tutawafikia na tunawashukuru sana wateja wetu kwa kutuunga mkono na tunawakaribisha ambao hawajajiunga na familia ya Vodacom kujiunga na kupata huduma bora kwa gharama nafuu, ” anasema Saleh.

Vodacom ina mtandao wa maduka 84 nchi nzima na wakala mbalimbali wakuuza bidhaa zake nchini na duka lililofunguliwa leo ni la 5 kufunguliwa katika wilaya ya Temeke.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents