Tragedy

Mke wa zamani wa Afande Sele, Mama Tunda afariki dunia

Aliyekuwa mke wa Afande Sele, Asha maarufu kama Mama Tunda, amefariki dunia.

10593347_546361882132195_621896920_n
Marehemu Mama Tunda

Taarifa hiyo imetolewa na Afande Sele kupitia ukurasa wake wa Facebook: Nimefiwa na mzazi mwenzangu (Asha) /mama wa wanangu (mama Tunda) ..ni pigo kubwa kwangu na wanangu. Sisi ni waja wa mwenyezi mungu na hakika kwake tutarejea; mungu ampumzishe pema.

1596915_331834436978493_2047405780_n

Wasanii mbalimbali wametuma salamu zao za rambirambi kwa Afande Sele.

Shilole

Pole kaka Afandesele! Kwa kufiwa ma mkeo mama tunda! Najua inaumaa kias gani! But Mungu yu pamoja nawe katika kipindi hiki kigumu

Lameck Ditto

Nimepokea kwa huzuni sana kifo cha aliyekuwa mke wa @afandeseletz ( Mama Tunda ). Pumzika kwa amani Mama Ndigi wangu.”.

Profesa Jay

Nimezipokea kwa mshtuko na simanzi kubwa sana taarifa za kufariki kwa mzazi mwenzie na @afandeseletz ASHA au MAMA TUNDA usiku wa kuamkia leo .. Pole sana kamanda wangu na Mwenyezi Mungu akutie Nguvu zaidi katika kipindi hiki kigumu, Ndugu zako tuko pamoja sana na wewe!! R.I.P MAMA TUNDA, Mungu alitoa na Mungu ametwaa jina la Bwana LIHIMIDIWE ..Amen

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents