Tragedy

Mke wa rapper Noorah, Camila afariki dunia

Mke wa rapper Noorah, Camila Kingwalu amefariki dunia jana nyumbani kwao Morogoro baada ya kuugua kwa muda mrefu.

11008208_1566860043566743_2093446419_n

Akizungumza na Bongo5, ndugu wa karibu wa marehemu ambaye hakutaka kutajwa jina lake, amesema Camila baada ya kuanza kuugua alirudi nyumbani kwao mpaka mauti yalipomkuta hapo jana.

“Kweli amefariki alikuwa kwao Morogoro na bado haikujulikana alikuwa anaumwa nini na mume wake naye anaumwa yupo kwao Shinyanga,” amesema.

20150303014602
Marehemu Camila

“Kwahiyo msiba upo Morogoro, kuna mtu ambaye anaelekea Morogoro sasa hivi akifika kule tutajua kila kitu. Morogoro alienda muda kidogo baada ya kuachana na mume wake. Baada ya kuachana, Noorah akaenda kwao na mke wake akaenda kwao. Hawakubahatika kuwa na watoto,” ameongeza.

“Marehemu alikuwa anaitwa Anna Kigwalu lakini baada ya kuolewa na Noorah akabadilisha jina na kuitwa Camila.”

Tunampa pole Noorah kwa msiba huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents