Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Michezo

Mke wa Michael Essien anunua klabu FC Como ya nchini Italia

By  | 

Mke wa aliyekuwa mchezaji wa Ghana Michael Essien ameinunua klabu ya ligi ya tatu Como ,kulingana na  taarifa ya klabu hiyo.

Akosua Puni Essien ameripotiwa kulipa pauni 206,000 katika mnada wa klabu hiyo iliofilisika.

Mmiliki mpya na timu yake sasa ana mpangowa kuimarisha kikosi cha kwanza pamoja na ile timu ya vijana kukuwa.

Wataweka juhudi za kuifanya kurudi katika Serie B na kukuza vipaji vya vijana waliomo.

Puni Essien amejielezea kuwa mfanyibiashara ,mshauri, mtu anayependa kusaidia na mama wa watoto watatu.

Como imeshiriki mara kadhaa katika ligi ya daraja la kwanza ya Seria A ,ikiwa imecheza sana kati ya 1984 hadi 1989 na hivi majuzi ikiwa 2002-2003 ambapo walishushwa daraja baada ya msimu mmoja.

Walishushwa daraja hadi ligi ya daraja la tano baada kufilisika.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW