Bongo Movie

Mke wa Kingwendu abakwa akiwa amelewa, azungumzia hatua anayoichukua

Baada ya mke wake kudaiwa kubakwa Alhamis iliyopita (July 24), muigizaji maarufu wa filamu za vichekesho nchini Kingwendu amesema atahakikisha mtu aliyehusika anapelekwa kwenye vyombo vya sheria.

Kingwendu.._full

Kingwendu ambaye alikuwa safarini wakati tukio hilo linatokea,ameiambia Bongo5 kuwa anajiandaa kupanda mahakamani baada ya mke wake kufanyiwa kitendo hicho cha kinyama wakati akiwa amelewa.

“Kama ulivyosikia hiyo habari, mimi nilikuwa sipo ndo nimerudi jana, nataka nianze kufuatilia sheria sema sasa hivi nimefiwa na dada yangu tunapeleka msiba kijijini na baada ya hapo ninapumzika kesho tu halafu ninasafiri Nairobi, nikirudi Nairobi tarehe tano kuanzia tarehe sita ndo naanza kufuatilia,” amesema Kingwendu.

“Kutokana na kitendo alichokifanya na mimi nimejisikia vibaya, inanibidi nimtafute huyu bwana nimpate ili nimpeleke mahakamani, mke wangu bado niko naye, sema huyu jamaa aliyefanya unyamaa huu yupo jirani. Mke wangu alikuwa amelewa na jamaa naye alikuwa amelewa. Mke wangu sijui alikuwa anatoka wapi saa tano usiku ndo akakutana na huyo jamaa, majirani ndio walivyoniambia hivyo, walinipigia simu wakati nipo Shinyanga huko.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents