Burudani

Mixtape ya kushtukiza ya Drake ‘IYRTITL’ kuuza kopi zaidi ya laki nne katika wiki ya kwanza

Surprise ndio mpango kwa sasa. Mixtape ya kushtukiza ya Drake, If You’re Reading This It’s Too Late iliyoachiwa usiku wa Alhamis, inatarajiwa kuuza kopi zaidi ya laki nne katika wiki yake ya kwanza kwa mujibu wa Billboard.

10986171_1565919690322155_539456075_n

Mixtape hiyo yenye nyimbo 17 inaweza kukamata nafasi ya kwanza kwenye chart ya Billboard 200 kwa kuuza zaidi kuliko soundtrack ya filamu ya Fifty Shades of Grey.

HITS Daily Double inakadiria kuwa mauzo yanaweza kufikia hadi 500,000 katika wiki yake ya kwanza.

Hayo yatakuwa mauzo makubwa zaidi katika wiki ya kwanza kwa album ya rap tangu ile ya Eminem, The Marshall Mathers LP 2 iliyokamata nafasi ya kwanza November 2013 kwa kuuza kopi 792,000.

“IYRTITL will become Drake’s fourth consecutive No. 1 debut following Thank Me Later (2010), Take Care (2011), and 2013’s Nothing Was the Same, which opened with 658,000 copies,” wameandika mtandao wa rapup.

“By comparison, Beyoncé’s 2013 surprise album sold 617,000 in its first three days on iTunes.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents