Burudani

Miss Universe Hellen atajwa kwenye jarida la Forbes Afrika kama mjasiriamali bilionea wa siku za usoni

Miss Universe Tanzania 2010, Hellen Dausen ambaye pia ni mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa Nuya’s Essence pamoja Edwin Bruno wametajwa katika jarida la Forbes Afrika kama wajasiriamali wenye umri wa chini ya miaka 30, wanaopewa kipaumbele kuwa mabilionea siku za usoni.
CjmW73ZXEAAG4C4
Kila mwaka jarida hilo hutoa orodha ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 30, wajasiriamali ambao wana nafasi ya kuwa mabilionea hapo baadaye.

Kupitia ukurasa wa twitter Hellen aliandika.

CjsYt_eVEAAe1Ov

Pia Bruno ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Smart-code inayotoa huduma ya usomaji wa magazeti kwa njia ya mtandao. Kampuni ya Nuya’s Essence, ni Nuya kampuni inayotengeneza bidhaa za ngozi na vipodozi.

Majina ya wajasiriamali hao yalikusanywa na kuandaliwa na mhariri wa Forbes Afrika Ancillar Mangena ambaye naye ana umri chini ya miaka 30.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents