Habari

Miss TZ afutiwa mashitaka

Mahakama ya Wilaya Kinondoni, imemfutia mashitaka Mrembo wa Tanzania, Miriam Gerald, baada ya mlalamikaji kuiambia mahakama kuwa hana mpango wa kuendelea na kesi aliyofungua.

Miriam pamoja na rafiki yake wa kiume, Kennedy Victor wamefutiwa mashitaka yaliyokuwa yanawakabili ya kumshambulia Shaaban Moshi kwa vitu vyenye ncha kali wakati shitaka la pili, ni kufanya uharibifu wa mali yenye thamani ya Sh720,000.

Hakimu waliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Kwey Lusemwa aliwaambia washtakiwa kuwa wako huru baada ya mlalamikaji kuonyesha kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Awali, Mwendesha Mashtaka Mrakibu wa Polisi, David Mafwimbo alisema mahakamani hapo kuwa mlalamikaji ametoa taarifa ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi na akaagiza iondolewe.

Mrembo huyo alitwaa taji hilo, Oktoba 2, 2009 kwenye Ukumbi wa Mlimani City lakini alifanya vibaya kwenye mashindano ya dunia yaliyofanyika Afrika Kusini mwishoni mwa mwaka jana.

Akizungumza jana, Mratibu wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga alisema: “Niliwaambia Watanzania tuiachie mahakama ifanya kazi yake na leo hii ukweli umeonekana.

“Mimi siamini kama hili lilikuwa na ukweli ndani yake, ni mambo ya kupandikiza lakini tuyaache imeshaamriwa hivyo…,” alisema Lundenga.

“Watu wanahukumu Miss Tanzania, lakini sivyo, sisi tunakaa na warembo muda mfupi sana, akitwaa taji, tunamtumia pale tunapomuhitaji na baada ya hapo anaendelea na maisha yake hatuwezi kumbana muda wote, sasa ni akili za wao wenyewe wajitambue nafasi yao.

Lundenga ambaye alirejea kuwataka radhi mashabiki wa urembo, aliwataka warembo kujitambua nafasi yao badala ya kufanya mambo yasiyokuwa na maana na kuharibu taswira nzima ya mashindano ya urembo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents