Events

Miss Tanzania kuanza kazi mwezi ujao

Miss TanzaniaMiss Tanzania Richa Adhia ataanza kufanya kazi za jamii mapema mwezi Februari na Machi kama ni sehemu ya kazi zake anazotakiwa kufanya kama mrembo. Mratibu wa Miss Tanzania Hashimu Lundenga alisema kuwa baada ya mapumziko ya sikukuu tunaanza kazi rasmi na mrembo wetu kama ni sehemu ya kazi zake za jamii

Miss Tanzania

 

Na Clara Alphonce

 

 

 

Miss Tanzania Richa Adhia ataanza kufanya kazi za jamii mapema mwezi Februari na Machi kama ni sehemu ya kazi zake anazotakiwa kufanya kama mrembo.

 

 

 

Mratibu wa Miss Tanzania Hashimu Lundenga alisema kuwa baada ya mapumziko ya sikukuu tunaanza kazi rasmi na mrembo wetu kama ni sehemu ya kazi zake za jamii anazotakiwa kufanyanya kama mrembo.

 

 

 

Baada mapumziko ya Sikukuu ya Krismasi na mwaka Mpya tumeona sasa tunaanza kazi rasmi kwa mrembo wetu kufanya kazi za jamii ambazo alikuwa ameziacha alipokwenda china kwenye mashindano ya Dunia�� alisema Lundenga.

 

 

 

Alisema pia, kilichowafanya wakae kimya toka mrembo huyo arejee kutoka China ni kutokana na watu kumpania sana mrembo huyo kwa kuwa watu walikuwa awamkubali toka avyotangazwa kuwa miss Tanzania.

 

 

 

Sisi tuliona tukae kimya kwa sababu watu walikuwa wamemuhukumu kabla hata yeye ajasema nini kilichomfanya ashindwe kufanya vizuri katika mashindano hayo na yote kwa kuwa alikua akubaliki kuwa miss Tanzania japo anavigezo vya kuwa miss Tanzania�� alisema Lundenga.

 

 

 

Alisema kwa sasa anaongea na wadhamini wa miss Tanzania ilikuhakikisha kuwa Richa anafanya kazi nyingi za jamii kwa kipindi hichi kifupi kabla awajaanza mchakato wa kuanza mashindano.

 

 

 

Source: Mwananchi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents