Burudani

Miss Tanzania 2014 mpya Lilian Kamazima naye awekwa kwenye kitimoto

Hatuna kazi za kufanya ama Watanzania tunapenda tu kulalamika? Katika ambacho kamati ya Miss Tanzania ilianza kuhisi imemaliza skendo ya Miss Tanzania baada ya Sitti Mtemvu kutangaza kujiuzulu, wahusika wataendelea kuwa na ‘sleepless nights’ kwa mara nyingine tena!

Miss Tanzania 2014 Lilian
Miss Tanzania 2014 Lilian Kamazima

Baada ya taji la Miss Tanzania kuvishwa kwa mshindi wa pili, utata mwingine umeibuka baada ya mrithi huyo, Lilian Kamazima kudaiwa kuwa si raia wa Tanzania. Jana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kulikuwa na taarifa zinazodai kuwa Lilian siyo raia wa Tanzania na kwamba anatokea Rwanda.

Akizungumzia tuhuma hizo, Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ndiyo waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Hashim ‘Uncle’ Lundenga alisema tuhuma hizo kuhusu Lilian siyo kweli.

“Sisi tunajua Lilian ni Mtanzania, tunaangalia cheti cha kuzaliwa alichotuletea kamati yetu ambacho kinaonyesha alizaliwa Tanzania, pia ni Mtanzania, hayo yanayosemwa kwamba Lilian siyo Mtanzania hatuyajui kabisa,” alisema Lundenga.

Pia Lundenga alisema kitendo cha Sitti Mtemvu kujivua taji la Miss Tanzania 2014 kumemnyima sifa ya kuendelea kushikilia taji la Miss Temeke na lile la Kitongoji cha Chang’ombe.

“Sitti amevua taji la Miss Tanzania maana yake ni kwamba hata lile la Miss Temeke 2014 na lile la Miss Chang’ombe 2014 ambayo ndiyo alikuwa mshindi kabla ya kushinda lile la taifa, ameyavua pia,” alisema Lundenga.

Sitti aliingia katika kashfa ya tuhuma za kudanganya umri baada ya nyaraka zake mbalimbali kuonyesha amezaliwa 1989 na siyo 1991 kama alivyowasilisha kwenye kamati ya Miss Tanzania.

Kwa mujibu wa sheria za mashindano hayo, mshiriki anatakiwa awe na umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 24.

Mwandaaji wa mashindano wa Miss Temeke, Ben Kisaka alisema, “Waliotoa taarifa ya Sitti kujivua taji ni kamati ya Miss Tanzania, hivyo wao ndiyo wanapaswa kutoa taarifa zingine kuhusu taji la Temeke.”

Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents