Burudani

Miss Tabata kunyakua mil 1

 

miss_Tabata_final2

Miss Tabata 2011 atapatikana leo katika ukumbi wa Da’ West Park , Tabata ambapo mshindi huyo atazawadiwa shilingi milioni moja.  Mratibu wa shindano hilo linaloandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts, Joseph Kapinga, amesema jana kuwa mshindi wa pili atapata shilingi laki

 

tano na wa tatu laki  tatu. Mshindi wa nne na watano watapata shilingi laki mbili kila moja. Washiriki wengine watakaoingia kumi bora watazawadiwa shilingi laki moja kila moja.  Warembo waliyosalia watapata kifuta jasho cha 50,000/- kila moja. Warembo 21 wanatarajiowa kushiriki kwenye kinyang’anyiro hicho ambapo bendi maarufu nchini African Stars “Twanga Pepeta” itatumbuiza kwenye shindano hilo ambalo ni kivutio cha wengi  jijini. 

miss_tabata_final

 

Washiriki ni Marion Augustino (19),  Neema Marwa  (18), Catherine Julius (20), Lilian William (20), Godliver Mashamba (22) na Dorice Mutabingwa (21).  Wengine ni  Sweetlily Suleiman (21),  Maria John (21), Happyness Emmanuel (18), Cresensia Haule (20), Mariam Manyanya (21),  Agustina Mshanga (20), Nasra Salim (21),  Faiza Ally (19) na  Edina Mnada (21).

Pia wamo  Angela Fortunatus (21),  Lucia Joseph (20),   Lilian Brayson (22),  Rita Mvungi  (21) na Willieth Wilson (22). Miss Tabata 2011 imedhaminiwa na Dodoma Wine, Vodacom, Redds Original,  Integrated Communications, Paris Pub, Fabak Fashion, Freditto Entertainment, Chicken Hut, Travel Partners, Ben Expedition, Screen Masters, Sean Entertainment, Michuzi blogspot, Anech Stationary na Vayle Springs

Consolata Lukosi ndiye mrembo anayeshikilia taji la Miss Tabata.  Mrembo huyo alikuwa nambari tatu mwaka jana kwenye shindano la taifa Vodacom Miss Tanzania  kabla ya kushinda taji la Redds Ambassador. Mashindano hayo ya urembo yanaandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents