Burudani

‘Miss Koi Koi’ ya Ommy Dimpoz imevuja, amtupia lawama Manecky

Wakati ambapo mashabiki wa Ommy Dimpoz wameipokea kwa furaha ile inayoonekana kama ngoma yake mpya, kitu kimoja kinaonekana hakiko sawa.

f6366c46837111e3a15212b173eacbf4_8

Kwa mujibu wa hitmaker huyo wa Tupogo, Miss Koi Koi si wimbo uliokuwa umepangwa kabisa kutoka. Staa huyo ambaye jina lake halisi ni Omari Nyembo, amesema amesikitishwa na kitendo cha producer wa wimbo huo, Manecky kuuachia bila idhini yake.

Ommy ameiambia Bongo5 kuwa, Miss Koi Koi uliosambaa leo, ni wimbo aliourekodi zaidi ya miaka miwili iliyopita katika wiki ambayo tuzo za KTMA zilikuwa zikitolewa na wimbo wake wa kwanza, Nai Nai kumpa ushindi.

Ommy amesema baada ya kuurekodi wimbo huo alibaki na demo yake tu lakini haukuwa miongoni mwa nyimbo alizokuwa anatarajia kuja kuziachia na kwake anauona kama umepitwa na wakati. Amesema wimbo uliotoka sasa umefanyiwa marekebisho na hivyo kumfanya apate jibu kuwa producer Manecky wa AM Records alidhamiria kuuvujisha.

Umeusikiliza wimbo huo? Unahisi ni wimbo wa kawaida kama Ommy anavyouchukulia?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents