Tragedy

Miss Honduras aliuawa kwa risasi wakati akimkimbia boyfriend wa dada yake

Miss Honduras aliuawa kwa kupigwa risasi wakati alipokuwa akijaribu kumkimbia boyfriend wa dada yake, polisi wamesema saa chache baada ya mwili wake na wa dada yake kupatikana.

Miss_Honduras_World_Maria_Jose_Alvarado_01_0

Maria Jose Alvarado, 19, aliyekuwa anatarajia kwenda London kwaajili ya shindano la urembo la Miss World, alipotea pamoja na dada yake Sofia Trinidad Alvarado siku sita zilizopita.

799b868aca679bb5d1dd63b56996caac1d187651
Polisi wa Honduras wakiwa wamemshikilia, Plutarco Ruiz — boyfriend wa dada yake na Miss Honduras

Gazeti la La Prensa limedai kuwa polisi wanachunguza endapo mpenzi wa Trinidad, Plutarco Ruiz, alimpiga risasi Sofia Trinidad kichwani baada ya kuingiwa na wivu alipomuona akicheza muziki na mwanaume mwingine.

Baadaye alimpiga Maria risasi mbili mgongoni alipokuwa akijaribu kukimbia. Polisi wamesema miili yao ilikutwa imezikwa pembeni mwa mto Aguagual uliopo kwenye mji wa Arada.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents