Burudani

Mimi ni rapper mwepesi kufananishwa na Fid Q – Nay wa Mitego

Nay wa Mitego amesema yeye ni rapper mwepesi kufananishwa na Fid Q na in fact hukasirika kusikia Ngosha anafananishwa na rapper mwingine hapa Bongo.

Ni kwasababu Nay anaamini uwezo wa Fid kwenye hip hop ni wa sayari nyingine.

“Simfananishi na rapper yeyote Bongo, sitaki, huwa nakasirika nikisikia wanamshindanisha na fulani, sipendi, najua hana mwenzake sijui huko mbeleni, Fid Q,” Nay alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio.

“Simfananishagi na rapper yeyote wa Kibongo, nakasirikaga kusikia wanamfananisha na msanii mwepesi, rahisi kama mimi au kama nani hao, please. Sisi wengine tupo sababu ya biashara, tunafanya tuna mashabiki sawa lakini kuna watu ambao wanafanya muziki wao ambao waliamua kufanya ukawa huko na wana heshima zao. Msifanye hivyo, na tena nikisikia East Africa mnamfananisha Fid Q na msanii flani, kuna siku ntakuja kuandamana,” aliongeza.

Kwa upande wake Fid Q baada ya kusikia kauli ya Nay, aliandika kwenye Instagram, “wewe sio mwepesi kaka @naytrueboy – so yawezekana kabisa na wao wakawa na vigezo flani special vinavyowapelekea wadau kunilinganisha au hata kunipima nao.. yote na yote.. ubarikiwe sana na asante sana kwa #LoveYaHelaYote.”

Wasanii wengine aliowataja kuwakubali ni Sugu, Mr Blue, Mwana FA na yeye mwenyewe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents