Burudani

Mimi ni msanii wa Hip Hop bongo mwenye video nyingi – Kala Jeremiah

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Kala Jeremiah amesema huwenda akawa yeye ni msanii wa Hip Hop mwenye video nyingi bongo kuliko wengine.
Kala

Rapa huyo ameiambia Bongo5 kuwa katika maisha yake ya muziki ni wimbo mmoja tu ambao haukuwa na video.

“Mimi siwezi kutoa wimbo bila video, katika muziki wangu wote nilitoa wimbo mmoja tu bila video, nadhani mimi ni msanii wa Hip Hop mwenye video nyingi, mpaka sasa nina video 16 yaani anaweza kuchukua hata tuzo ya msanii wa Hip Hop mwenye video nyingi,” alisema Kala.

Kala ambaye ni baba wa mtoto mmoja aitwae Alama, amesema anajipanga kuachia wimbo wake mpya mwezi ujao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents