Burudani
Mimba imekua kubwa: Picha hii yathibitisha rasmi Zari ni ‘mama kijacho’
Zari the Bosslady yupo nchini alikokuja kumsalimia mpenzi wake, Diamond Platnumz.
Hivi karibu kulianza kuzuka maneno kutoka kwa baadhi ya watu kuwa wana mashaka na kama kweli mrembo huyo wa Uganda ni mjamzito.
Lakini kwa mujibu wa picha iliyosambaa mtandaoni leo, ni kweli Zari anatarajia kuwa mama kwa mara ya nne.
Kwenye picha hiyo, Zari anaonekana akiwa amevaa gauni jekundu ambalo linaonesha wazi jinsi mimba yake ilivyokuwa.
Picha hiyo imevuta hisia za wengine akiwemo Ray C aliyeipost kwenye Instagram na kuwataka mashabiki wake wamtaje baba wa mtoto huyo.