Burudani

Millard Ayo awa Mtanzania wa tatu kufikisha followers milioni 1 Instagram

Mtangazaji wa nguvu Millard Ayo kutoka Clouds Fm, amekuwa Mtanzania wa tatu kufikisha followers milioni moja kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram. Hadi leo amefikisha 1,007,912.

Millard-Ayo

Host huyo wa kipindi maarufu cha Amplifaya amekuwa wa tatu kufikisha idadi hiyo baada ya Wema Sepetu, ambaye alifikisha idadi hiyo mwezi huu wa Novemba. Mpaka sasa Wema amefikisha 1,077,859. Mtanzania wa kwanza kufikisha idadi hiyo alikuwa Diamond Platnumz ambaye kwa sasa ana 1,311,940.

ayo insta

Mastaa wengine ambao wanakaribia kufikisha followers milioni moja ni pamoja na Vanessa Mdee ambaye hadi sasa amefikisha 918,521.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents