Milioni Kumi ya Tatu Yagawiwa

 

Mshindi wa tatu wa Milioni Kumi, Dr. Licky Abdallah mwenye umri  wa miaka 52, wa bahati nasibu ya kipekee ya SUPA PESA amekabidhiwa hundi ya fedha hizo leo jijini Dar es salaam.

Dr. Licky Abdallah ambaye ni mkazi wa Dar es Salaam, ni mkurugenzi wa kampuni ya Malagarasi Tours and Safaris na pia ni mchambuzi maarufu wa wa mpira wa mguu (soka ) hapa jijini. Alipokea hundi hiyo kwa furaha na kusema kwamba alikuwa akichukulia kama utani pale ambapo alisikia kuhusu droo hii ya Supa Pesa na kushiriki kama utani.

‘Ilitokea kama bahati kubwa pale ambapo nilipigiwa simu na kituo cha radio  Clouds FM kujulishwa kuhusu ushindi wangu. Kiukweli nilijawa na furaha sana. Pesa hizi nitaziongezea kwenye mtaji wa biashara yangu na pia kumtunuku zawadi binti yangu ambaye alinishawishi kushiriki droo hii ya Supa Pesa.’ Alisema Dr. Licky.
Msemaji wa Supa Pesa, Bi. Natasha Issa, kwenye zoezi la kumkabidhi mshindi huyo hundi yake, amesema kwamba washindi wanazidi kumiminika kila siku kutoka kila kona ya Tanzania. Aliwataka watanzania wengi zaidi  kushiriki droo hii ambapo kila siku kunapatikana washindi watatu wa milioni moja, na Mshindi mmoja wa Milioni Kumi kila wiki.

Bi.Natasha aliongezea kwa kusema,‘Kushiriki droo ya Supa Pesa ni rahisi, inahitaji kutuma ujumbe mfupi wenye neno SUPA kwenda namba 15777. Hii inakuwezesha wewe kuingia moja kwa moja kwenye ushindani wa shilingi milioni moja kila sikui na ukishiriki kutuma Ujumbe mfupi wa simu zaidi ya mara nne basi utakuwa kati ya washindani wa milioni kumi kila wiki,’

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents