Michuano ya U 17 Yasogezwa Mbele

MICHUANO ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya miaka 17 yamefutwa baada ya Shirikikisho la soka la Afrika Mashariki na kati ‘CECAFA’ kuandika barua kwa TFF hayotafanyika kutokana na kukosa fedha za kuendeshea mashindano hayo.

MICHUANO ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya miaka 17 yamefutwa baada ya Shirikikisho la soka la Afrika Mashariki na kati ‘CECAFA’ kuandika barua kwa TFF hayotafanyika kutokana na kukosa fedha za kuendeshea mashindano hayo.
Mashindano hayo ambayo yalikua yaanze Desemba 6-20 hayatafanyika tena hadi mwakani na kwa sasa timu hiyo ya Serengeti Boys itafanya ziara Mikoani kwa ajili ya kujiandaa na mashindano mengine pamoja na kuunda timu ya Taifa.
Akizungumza na Waandishi wa habari jana Katibu mkuu wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania ‘TFF’ Fredrick Mwakalebela alisema mashindano yameahilishwa hadi mwakani kutokana na CECAFA kukofa wadhamni.
“TFF imepata barua kutoka CEAFA inayotoa taarifa kuwa mashindano hayatakuwepo mwaka huu hadi hapo mwakani nakudai shirikisho lina dola 25,000 tu ambazo haziwezi kutoshereza gharama za mashindano,” alisema Mwakalebela.
Alisema kutokana na taarifa hizo wao kama TFF wameamua kuiandalia timu ziala ya mikoani kwaajili ya mechi za kirafiki ambazo zitamsaidia kocha kuwatengeneza vijana kwaajili ya timu ya taifa.
Kati ya Jumatano na Alhamisi timu itaenda Dodoma kucheza na Police dodoma, Morogoro watacheza na Mtibwa Sugar na badaaye kurudi Dar es salaam na kucheza mchezo mmoja na timu yeyote ya Ligi Kuu Baada ya hapo kambi itavunjwa rasmi.
“Hatuvunji kambi leo kwakua lengo letu ni kuwaandaa vijana wawe wachezaji wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’, hivyo tumeamua kuwaandalia mechi za kirafiki na timu za Ligi Kuu ili kuwaongezea uwezo na hali ya kujiamini uwanjani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents