Burudani

Miaka 11 tangu Father Nelly afariki: JCB akumbushia kifo cha kilivyokuwa na pengo lake kwenye hip hop

Leo ni miaka 11 tangu kifo cha rapper wa kundi la Xplastaz, Father Nelly.

Rapper huyo alifariki baada ya kuchomwa kisu March 29, 2006 jijini Arusha.
Jumatano hii, nimezungumza na rapper JCB aliyekuwa rafiki yake wa karibu ambaye anatukumbusha jinsi kifo cha Nelly kilivyotokea.

“Mahali anapokaa kulikuwa na ugomvi kati ya jirani yake na rafiki yake sasa akaenda kama kuingilia kwamba ‘ebana inakuaje’ basi yule jamaa ambaye ndiye muuaji akamuambia Father Nelly ‘na wewe unataka sio’ akamchoma visu vingi sana pale pale bana. Kumchoma visu jamaa akakimbia watu wakamkimbiza Father Nelly Mount Meru hospitali akakaa siku ya kwanza, siku ya pili ndio siku kama ya leo akafariki kwa maumivu makali sana,” amekumbia JCB.

JCB amesema Father Nelly ni mmoja wa watu walioanza kurap mapema zaidi huko Arusha kuanzia mwaka 1992/93 akiwa na umri mdogo kabisa.

“Watu wa Arusha watakuwa wanammiss sana sababu wao [Xplastaz] ndio walikuwa wa kwanza kuipeleka game ya Arusha Dar es Salaam huko, kuipeleka nje ya Tanzania. Nadhani Xplastaz na Mr 2 ndio waliweza kuwa watu wa kwanza kwenda kurap nje ya Tanzania,” anasema JCB.

JCB anasema Arusha haitokuja kumsahau rapper huyo na kwamba miaka ya nyuma siku kama ya leo kulikuwepo na desturi ya kufanya kongamano la kumkumbuka, kitu ambacho kimepotea kwa sasa.

JCB aliwahi kuandika wimbo maalum wa kumkumbuka rapper huyo pamoja na watu wengine waliotangulia mbele ya haki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents