Burudani

Mheshimu meneja wako upate miaka mingi ya maisha ya muziki – Said Fella

Meneja wa TMK Family pamoja na Mkubwa na Wanawe, Said Fella amewataka wasanii wa muziki kuwaheshimu mameneja wa muziki kwani ndio watu wanaofanya kazi kubwa kwenye muziki wao.

11380211_920325464693119_1982105870_n

Fella ameiambia Bongo5 kuwa wasanii wanatakiwa kuwachakulia mameneja kama sehemu muhimu katika muziki wao.

“Mimi naamini ukiamua kujitoa kwenye kazi na ukasema hii ni kazi yangu, lazima kazi inakuwa bora,” amesema Fella. “Kwahiyo ninaweza nikawasisitizia hao mameneja wenzangu wanaojiona wao na kujiita mameneja kwamba wajitahidi kuwatengeneza wasanii wao ili wawe wazuri zaidi. Halafu na vile vile wasanii wanatakiwa kuwachukulia mameneja wao kama part ya muziki wao.

Lakini wasiseme meneja ni shabiki wa muziki wao. Ukijifanya msanii ukamuona meneja mpambe wako au rafiki wa muziki wako mameneja watakuacha. Lakini ukiwaheshimu na kuwapa nafasi zao utafika mbali sana,” amesisitiza Fella.

“Mimi wasanii wangu wamenichukulia ni mtu wao muhimu ndo maana mimi najitahidi kwa hali na mali ili kuonekana meneja bora kutokana na kufanya kazi iliyo bora. Kwahiyo meneja amtegemee msanii na msanii amtegemee meneja.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents