Habari

Mhariri Mtendaji na mwandishi wake wa gazeti la Mwananchi waitwa polisi

Mhariri mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Frank Sanga na mwandishi wake, Elias Msuya wameitwa na polisi kuhojiwa kuhusu makala iliyochapishwa na gazeti hilo kuhusu utendaji wa jeshi hilo.
mwandishi
Hiki ni kipande cha gazeti cha makala hiyo

Wakati Msuya alipigiwa simu jana na kuhojiwa leo asubuhi kuhusu makala aliyoandika, Sanga ameitwa leo na tayari ameondoka ofisini kwake kwenda Kituo Kikuu cha Polisi kuitikia wito huo.

Makala hiyo ya uchambuzi yenye kichwa cha habari “Polisi na Hofu ya Watawala Kuondoka Madarakani”, ilichapishwa na gazeti hilo jana.


Source: Mwananchi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents