Habari

Mhadhiri chuo kikuu akamatwa na TAKUKURU kwa kuomba rushwa ya ngono

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Kinondoni inamshikilia Mhadhiri Msaidizi wa Chuo cha Taifa cha Usifirishaji (NIT), Samsoni Mhimbo (66) kwa kosa la kuomba rushwa ya ngono kutoka kwa mwanafunzi wa kike baada ya kumwekea mtego kwa lengo la kumpa alama nzuri katika mtihani wake.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ijumaa hii, Kaimu mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kinondoni, Dennis Manumbu, alisema awali mwanafunzi huyo alitoa taarifa ya kuombwa rushwa ya ngono na Mahimbo ili ampatie matokeo mazuri ya mtihani wa marudio (Supplementary Examination) alioufanya Januari 5, mwaka huu.

“Amekamatiwa katika nyumba ya kulala wageni ya Camp David iliyopo mwenge Mlalakuwa Dar es salaam, siku ya Alhamisi tarehe 12 mwezi wa kwanza mwaka 2017 majira ya alasiri. Mtuhumiwa bwana Mahimbo alikamtwa na Takukuru baada ya kuwekewa mtego kufuatia na taarifa iliyotolewa na mwanafunzi aliyekuwa akiombwa rushwa hiyo ili aweze kumpatia matokeo mazuri ya mtihani wa marudio,” alisema

“Natoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Takukuru ili kuweza kuzuia vitendo vya rushwa na kuwachukulia hatua za kisheria wale wote ambao uchunguzi utathibitisha kukabiliwa na tuhuma za rushwa ikiwamo rushwa ya ngono”.

Aidha Manumbu alisema rushwa ya ngono ni kinyume na kifungu cha 25 cha Sheria namba 11 ya mwaka 2007 ya Kuzuia na Kupambana na rushwa inayoeleza kuwa ni kosa kwa mtu kutumia mamlaka aliyonayo kumtaka mtu kimapenzi ili ampe upendeleo katika kumhudumia.

BY: Emmy MWaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents