Burudani

Mfahamu mchumba wa mwimbaji wa nyimbo za gospel kutoka Kenya Bahati

Msanii wa nyimbo za injili kutoka Kenya maarufu kama Kevin Bahati, kwa sasa anakila sababu ya kutabasamu baada ya hivi majuzi kuamua kumtambulisha kwa mashabiki wake mchumba wake.

Bahati ambaye kuna wakati aliwahi kutangaza wazi hadharani vile anavyomzimia mrembo wa filamu Bongo Elizabeth Lulu inaonekana alikuwa yuko serious na alichokisema. Kwani hata baada ya kumkosa Lulu mrembo ambaye yuko naye kwa sasa anafanana japo kwa umbali na Lulu.

Japo wengi wa mashabiki wa Bahati walitamani kuona couple ya Lulu na Bahati hilo halitaweza kutokea kwani Bahati amechukua mkondo mwingine na tayari anamchumbia kipusa mwingine tofauti.

Ikizingatiwa umarufu wa Lulu urembo wake unaoleta mvuto kwa mashabiki wake wa kiume kote Afrika Mashariki ikiwamo hapa nchini Kenya basi hakuna anayepinga Bahati aliufungua ukweli wa moyo wake juu ya mapenzi yake kwa Elizabeth Lulu. Lakini dua la kuku halimpati mwewe, dua la mashabiki kuhusiana na Bahati na Lulu, limeenda mvange.

Sasa Bahati anatamba mtaani na kisura ambaye hata si public figure, na ndio sasa kimwana huyo anauparamia utamu wa umaarufu wa staa huyo kutoka hapa Kenya.

Kipusa huyo ambaye anafahamika kama Diana Marua, kwa jina la utani ambalo Bahati amempa ni prayer partner. Mashabiki wa msanii Bahati wamefurahia couple hii, ambayo ndio couple mpya mjini kwa sasa. Kwa sasa bahati anatamba na ngoma mpya aliyomshirikisha msanii mkali wa gospel kutoka hapa Kenya pia Mr. Seen kwa jina Kumbekumbe.

Makala ya: Changez Ndzai ( Kenya)
Facebook: Changez Ndzai
Twitter : ChangezN
Instagram: changez_ndzai

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents