Michezo

Method Mwanjale arejea tena uwanjani

Mchezaji wa klabu ya Simba SC, Method Mwanjale anatarajia kuanza mazoezi katika kikosi hicho hii leo.

Beki huyo ambaye hucheza nafasi ya beki wa kati wa Simba, amerejea juzi akitoka kwao Zimbabwe ambako alikwenda baada ya kuwa majeruhi.

Mwanjale raia wa Zimbabwe amekuwa akisumbuliwa na maumivu yaliyomfanya kukaa nje kwa zaidi ya wiki mbili.

“Sasa yuko vizuri kabisa, siku zake za kupumzika zimeisha na ziada pia. Hivyo anaweza kuanza mazoezi,” zilieleza habari kutoka ndani ya Simba.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents