Michezo

Mesut Ozil atetewa na wakala wake baada ya Arsenal kupata kipigo 5-1

By  | 

Mchezaji wa klabu ya Arsenal Mesut Ozil anaamini analaumiwa bila msingi wowote kutokana na matatizo yanayoikumba klabu hiyo, wakala wake amesema.

Ozil, 28, alilaumiwa tena baada ya Arsenal kupokea kichapo cha 5-1 ugenini kwa Bayern Munich katika mechi ya hatua ya 16 bora Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya siku ya Jumatano.

“Ukosoaji ni kawaida mchezaji anapocheza vibaya,” Dkt Erkut Sogut aliambia BBC Sport.

“Lakini Mesut anahisi kwamba watu waangazii vyema uchezaji wake; na badala yake analaumiwa bure baada ya timu kupata matokeo mabaya.”

Ozil alijiunga na Arsenal kutoka Real Madrid mwaka 2013 kwa ada ya £42.4m iliyovunja rekodi ya klabu hiyo ya England.

Alitua Emirates akiwa an sifa za kuwa mmoja wa viungo wa kati wazuri sana duniani.

Lakini uchezaji wake karibuni umekosolewa sana.

Dhidi ya Bayern, alikamilisha pasi 20 pekee, ambazo ni sawa na alizokamilisha kipa wa Bayern Manuel Neuer.

“Bayern walidhibiti mpira 74% ,” alisema Sogut, ambaye pia ni wakili wa Ozil.

“Mchezaji ambaye ni nambari 10 uwanjani anawezaje kuunda nafasi iwapo hapati mpira?

“Katika mechi kama hizi watu humlenga zaidi mchezaji aliyegharimu pesa nyingi na anayelipwa pesa nyingi – na huyo ni Ozil. Lakini hawezi kulaumiwa kila wakati. Si haki.

“Soka ni mchezo wa timu na Arsenal kwa sasa hawachezi vyema kama timu. Kulikuwa na wachezaji kumi na mmoja uwanjani lakini Mesut ndiye anayelaumiwa. Je, ndiye aliyesababisha Arsenal kufungwa magoli matano?”

Source: BBC

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments