Habari

Meno ya tembo kutouzwa wala kuchomwa moto

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, amesema msimamo wa serikali ya Tanzania kwa sasa kuhusu meno ya tembo yaliyohifadhiwa nchini si kuyauza wala wa kuyachoma.

Hayo yamesemwa na waziri huyo wakati Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Alipoitembelea wizara hiyo Dar es Salaam Alhamisi hii, katika ghala la nyara za serikali kuona utunzaji wa meno ya tembo na changamoto zake.

“Msimamo wetu ni kama ule wa nchi za Kenya, Uganda, Zambia, Malawi na Msumbiji wa kutokuuza meno haya kwa sasa kwa sababu mbalimbali, ikiwemo utafiti. Vinasaba vya meno ya zamani vinaweza kutumika kubaini mambo mbalimbali ikiwemo utafutaji wa dawa ya magonjwa ya tembo,” alisema.

Aidha Waziri Maghembe alisema pia kuwa serikali kwa sasa haina mpango wa kuuza wala kuchoma meno hayo.

BY: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents