Habari

Meninah kufanya video ya ‘Kacopy Kapaste’ nchini Kenya

Msanii Meninah amesema anatarajia kushoot video ya wimbo wake mpya ‘Kacopy Kapeste’ nchini Kenya, wimbo ambao aliuzindua katika club ya Billicanaz wiki kadhaa zilizopita.

Meninah

“Naenda kushoot Nairobi Kenya ndio kule location itakapokuwa “, amesema Menina kupitia Power Jams ya EA Radio.

Meninah ameongeza sababu za kuamua kuifanya video mpya nje ya Tanzania.

“Kila siku zinavyoenda nataka ku invest makubwa zaidi katika muziki wangu sababu siwezi kuwa vile vile kama ilivyokuwa kwenye muziki wangu wa nyuma…mimi kama mimi nimeona kwanini nisifanye na madirector wa nje ili nipate idea na concept nyingine nje ya Tanzania ndio maana nikafikiria kufanya hivyo “.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents